Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya ametembelea chuo kikuu cha Al-Ameed na kukagua mkakati wake wa kupokea mwaka mpya wa masomo

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Ataba tukufu, kwa lengo la kuangalia maandalizi ya kuupokea mwaka mpya wa masomo, yanayo endana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, mazingira ya ugonjwa wa Korona na utekelezaji wa maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na kamati ya kupambana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

Amepokewa na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali na msaidizi wake pamoja na walimu wa kitivo cha udaktari na famasia.

Amesikiliza maelezo yao, na akaangalia maandalizi ya chuo na mikakati yake ya kuupokea mwaka mpya wa masomo, sambamba na kuangalia vifaa vya kufundishia, na njia za kuviboresha na kutumia ufundishaji wa kielektronik katika kipindi hiki cha janga la Korona, janga ambalo limebadilisha mfumo wa vitu vingi katika maisha ya watu hapa nchini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: