Kitengo cha kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kimezawadia watu (2100) walio jitolea kufanya kazi wakati wa ziara ya Arubaini.

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimewapa zawadi watu waliojitolea kufanya kazi pamoja nao wakati wa ziara ya Arubaini, ambao idadi yao ilifika watu (2100), waligawanywa sehemu tatu, kutoa huduma kwa mazuwaru, kuratibu na kusimamia matembezi na kutoa huduma za mambo ya afya.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Utoaji wa zawadi hizi unatokana na kuonyesha kutambua na kuthamini kazi zilizo fanywa na watu hao, ambao wamekuwa msaada mkubwa wa watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili katika kutekeleza majukumu yake wakati wa ziara ya Arubaini, wamefanya kazi kubwa katika sekta tofauti, ikiwemo sekta ya kuratibu na kusimamia utembeaji wa mazuwaru na mawakibu na kuhakikisha hakutokei msongamano wa watu, kuna waliofanya kazi kwenye sekta ya usafi na kuandaa sehemu za kupumzika mazuwaru pamoja na kuwapa mahitaji ya lazima wakati wa ziara, wamesaidia pia katika sekta ya afya, sekta ambayo ni muhimu sana kutokana na mazingira ya mwaka huu ya uwepo wa janga la maambukizi ya virusi vya Korona”.

Wafanyakazi wa kujitolea wameshukuru kupewa nafasi ya kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wakasema hii ni heshima kubwa kwetu, na kubwa zaidi ni kupewa zawadi na kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili, tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe afya na umri mrefu ili tuendelee kushiriki katika misimu mingine ya ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: