Tangazo la kuanza mwezi wa Rabiul-Awwal: Bendera nyekundu yapandishwa katika kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Baada ya kuisha miezi miwili ya huzuni Muharam na Safar, baada ya swala za Magharibaini za Jumapili (30 Safar 1422h), bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) imebadilishwa na kupandishwa bendera iliyo andikwa (Ewe mwezi wa bani Hashim), kama ishara ya kumaliza msimu wa huzuni wa miezi miwili Muharam na Safar na kuingia mwezi wa Rabiul-Awwal.

Mtu anaweza kuuliza, katika mwezi wa Muharam na Safar hatukuona bendera nyekundu bali tumeona bendera nyeusi kwa nini?

Jibu la swali hilo ni: Kupandisha bendera nyeusi kunamaanisha kuwa siku hizi ndio alizo uwawa mwenye kaburi hili, ndio maana huwa tunapandisha bendera nyeusi kwenye kubba la kaburi la bwana wa mashahidi Imamu Hussein na kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku za mwezi wa Muharam na Safar.

Bendera imepandishwa na kushuhudiwa na mamilioni ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) huku macho yao yakitokwa machozi na mazingira yao yakionyesha kusema: Ewe kiongozi wetu ewe Imamu wa zama, haujafika wakati wa kulipiza kisasi cha watu walio uwawa Karbala? Haujafika wakati wa kuondoa hii bendera nyekundu juu ya kaburi la babu yako Hussein? Lini tutasikia sauti ikiita (Yaa-lithaaraat Hussein)?
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: