Kwa ushiriki wa mafunzo ya kiangazi: Zaidi ya wanafunzi (400) wa udaktari wa meno wanahudhuria masomo katika chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel kimeanza kuendesha semina za majira ya joto kuanzia tarehe (17 Oktoba 2020m) kwa wanafunzi wake zaidi ya (400).

Dokta Nawali Almayali makamo rais wa chuo katika kitengo cha taaluma amesema kuwa: “Hakika uongozi wa chuo kikuu cha Alkafeel umeagiza kitivo cha udaktari wa meno kiandae mahitaji yote ya lazima, na wafungue maabara zote zilizopo ndani ya jengo la chuo pamoja na vituo vya nje vilivyo chini ya chuo hiki kwa ajili ya kufanikisha ufundhishaji wa semina za kiangazi kwa wanafunsi wetu, sambamba na kuheshimu masharti ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, kama yalivyo elekezwa na wizara ya afya”.

Akaongeza kuwa: “Chuo kinatilia umuhimu mkubwa kufundisha mambo ya lazima kwa wanafunzi yatakayo wawezesha kuongeza kiwango chao, na kuwafanya waweze kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu”.

Dokta Sarmadi Muhammad msaidizi wa kiongozi mkuu wa kitivo cha udaktari wa meno akasema kuwa: “Kitivo chetu kimeanza kuendesha semina za majira ya joto, zitakazo dumu kwa muda wa wiki sita, wakufunzi wanatumia ujuzi wao wote katika kufanikisha hilo, wamegawa wanafunzi katika makundi madogo madogo ili waweze kufaidika vizuri na kulinda usalama wao, aidha kitivo kimeunda jopo maalum la kupuliza dawa kumbi za madarasa na vifaa wanavyo tumia kusomea”.

Akaongeza kuwa: “Muda wa masomo utakua siku mbili katika wiki kwa kila kikundi, chini ya maelekezo ya wizara yaliyo tufikia, yatakayo wawezesha wanafunzi kupata mada zilizo pangwa”.

Tambua kuwa maabara za kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel zilisanifiwa na kutengenezwa kwa kufuata viwango bora vya elimu, zinasifiwa na kila mtu anaezitembelea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: