Kitabu cha (Shekhe wa wairaq) ni moja ya matolea makubwa ya kituo cha turathi za Karbala

Maoni katika picha
Miongoni mwa juhudi zake za kukusanya kila kinacho husiana na mji wa Karbala, kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimeangazia mmoja wa wanachuoni wa mji huu, naye ni Shekh Abdulhussein Twaharani Alhaairiy ajulikanae kwa jina la (Shekhe wa wairaq), kupitia moja ya machapisho ya kituo kwa anuani ya jina la Shekhe aliyetajwa.

Kitabu hicho ambacho ni katika uandishi wa Shekh Haamid Radhwaiy na tarjama ya Ustadh Hassan Ali Hassan Matwar kinazungumzia historia ya mwanachuoni mkubwa wa mji wa Karbala, ambae ni Shekh Abdulhussein Twaharani Alhaairiy, ambae ni kati ya watu wanne waliozungumzwa na muandishi wa kitabu cha Aljawahiri (r.a) kwa ijtihadi akiwa katika mimbari ya ufundishaji, na anamchango mkubwa katika ujenzi wa Ataba tukufu, alipambana na baadhi ya makundi yaliyo potea na akazuwia kuenea kwa makundi hayo, kutokana na utukufu wake watawala wa Othumaniyya walimpa jina la (Shekhe wa wairaq) wakimaanisha: Shekhe wa Iraq na Iran.

Kitabu kinamilango kumi na kunamlango ulioandikwa mabo ambayo hayakupata sehemu katika milango hiyo.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya kazi ya kukusanya kila kinacho husiana na turathi za mji wa Karbala, kimefanikiwa kuchapisha vitabu vingi na kukusanya taarifa nyingi za kitafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: