Kituo cha turathi za Najafu ni dirisha la kuhuisha na kusambaza turathi za Ahlulbait (a.s)

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Najafu ni moja ya sehemu za kufanya tafiti za turathi za Najafu, ni sehemu ya miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu pia, iliyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, kinacho husika na mambo ya taaluma na turathi kwa kufanya tafiti na kutengeneza faharasi pamoja na kusambaza mafundisho ya Ahlulbait (a.s).

Mkuu wa kituo hicho, Ustadh Ahmadi Ali Majidi Alhilliy ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Kituo kilianzishwa mwanzoni mwa mwezi wa Rabiul-Awwal mwaka 1441h, na kina idara nyingi, kinafanya kazi kubwa kwa baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuhakiki faharasi ya turathi za Najafu, na kufungua pazia katika kuangazia vitabu vya wanachuoni wetu watukufu, na kutoa matunda bora kwenye sekta ya turathi”.

Akabainisha kuwa: “Katika kuonyesha umuhimu wa viongozi na wanachuoni watukufu pamoja na kudhihirisha hazina zao zilizo fichika, kituo kimechapisha kitabu cha (Mustadraku Dhariáh) ambacho kinamambo ambayo hayakutajwa na Shekh Aghabazarka Twaharani katika maelezo ya kitabu cha (Dhariáh) hadi mwaka wa kifo chake (1389h), pamoja na kutaja rejea na sehemu vinakopatikana vitabu hivyo, akataja tarehe za uandikwaji wake na baadhi ya mambo yaliyomo, pamoja na yale yaliyo chapishwa katika nakala alizo andika kwa mkono, kituo cha faharasi kimekamilisha (mlango wa twahara) katika kitabu cha (Kuondoa giza katika sura ya sheria za kiislamu) cha shekhe Muhsin bun Murtadhwa A’sam aliyekufa mwaka (1238h) nacho ni kitabu cha dalili (istidlali), inawezekana kikawa na juzuu Arubaini, na kazi ya kusambaza uhakiki wa kitabu cha masaaili kiitwacho (Risalatu-Twaharah) cha shekhe Hilali Karkiy, ajulikanae kwa jina la ibun Minshaari Al-Aamiliy aliyekufa mwaka (984h)”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimeanzisha vituo vingi vya turathi, kama sehemu ya kuhuisha turathi za umma wa kiislamu, na kuvikabidhi kwa ajili ya wasomaji, wanafunzi, watafiti na wadau tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: