Madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kubadilisha mirija miwili kwenye moyo wa mgonjwa mwenye umri wa zaidi ya miaka thelathini

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kumtibu mgonjwa mwenye umri wa zaidi ya miaka thelathini aliyekuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo.

Dokta wa upasuaji wa moyo katika hospitali hiyo bwana Bashiru Akbinaar amesema kuwa: “Hakika jopo letu la madaktari limefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo kwa mgonjwa mwenye umri wa mika (33)”.

Akabainisha kuwa: “Tumefanikiwa kubadilisha mirija miwili ya kwenye moyo”.

Akaongeza kuwa: “Upasuaji wa moyo ambao tumesha fanya katika hospitali ya Alkafeel hadi sasa ni zaidi ya (400), na kiwango cha mafanikio ni asilimia (%98), mafanikio hayo yanatokana na vifaa tiba vya kisasa tulivyo navyo na madaktari mahiri”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inajitahidi kutoa huduma bora wakati wote kupitia vifaa tiba vya kisasa ilivyo navyo na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo hili limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti kila wakati, sambamba na kupokea wagonjwa ambao wapo katika hali mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: