Maahadi ya Quráni tukufu inashiriki kwenye nadwa ya utamaduni katika wilaya ya Hindiyya

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa nadwa zinazo fanywa, na kushiriki Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya, na kwa kushirikiana na kiongozi wa wilaya ya Hindiyya katika mkoa wa Karbala, jana siku ya Jumanne mwezi (2 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na tarehe (20 Oktoba 2020m) Maahadi ilishiriki katika nadwa ya utamaduni iliyokuwa inazungumzia uhai wa Mutume Muhammad (s.a.w.w) na namna ya kunufaika nae katika jamii.

Nadwa hiyo ilifanyika kwenye jengo la utamaduni chini ya uhadhiri wa Shekh Hamza Fatalawi, akazungumzia safari ya islahi iliyofanywa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa kutumia maarifa kubwa, eleza pia utukufu wa tabia zake zinazo endelea kuonyesha ubinaadamu wa hali ya juu hadi leo.

Akafafanua namna ya kunufaika na Mtume (s.a.w.w) katika kuleta maelewano (islahi) na kupambana na changamoto mbalimbali zinazo tukabili, ikiwa ni pamoja na changamoto za kijamii, kitamaduni na zinginezo.

Kiongozi wa Maqaam ya Hindiyya Ustadh Muntadhir Shafi ameishukuru sana Maahadi ya Quráni tukufu kwa kushiriki kwenye nadwa hiyo, na kila inacho fanya katika kusambaza elimu ya Quráni pamoja na turathi za Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: