Kuanza kazi katika mradi wa uwanja wa haram ya Saaqi

Maoni katika picha
Kitengo cha ujenzi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kazi ya kuweka marumaru, ambayo ni sehemu ya pili ya mradi wa ujenzi wa uwanja wa haram ya Saaqi, uliopo upande wa mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kusimama kwa muda wakati wa ziara ya Arubaini, awamu hii inakamilisha awamu zilizo tangulia upande wa kushoto wa haram ya Aljuud kwa anaye ingia katika malalo takatifu, sehemu hiyo ina ukubwa wa mita (850) takriban.

Kiongozi wa kazi za ujenzi katika kitengo hicho Mhandisi Muhammad Mustwafa Twawiil amesema kuwa: “Baada ya kumaliza kazi kwenye uwanja wa haram ya Aljuud, uliokuwa na ukubwa wa zaidi ya mita (1000), na eneo hilo kuanza kutumiwa na mazuwaru wakati wa kufanya ziara, na kusaidia kupunguza msongamano kwenye mlango wa Kibla, baada ya kumaliza ziara ya Arubaini watumishi wetu wameanza ujenzi sehemu hii inayo itwa (Saaqi), ambayo ujenzi wake wa chini ulikua umesha kamilika, pamoja na uwekaji wa nyaya za umeme, mabomba ya maji taka na safi”.

Akaongeza kuwa: “Kazi inayo endelea hivi sasa ni kuandaa tabaka la ardhi kwa kuweka ruva ili kuinua sehemu ya barabara, pamoja na kuweka uzio unao tenganisha eneo hilo na soko lililopo pembeni yake katika eneo lenye urefu wa mita (35) kwa kimo cha mita mbili, sehemu ya chini ya uzio huo imejengwa kwa mawe yenye kimo cha (sm 60), na sehemu ya juu kumewekwa vyuma vilivyo tiwa nakshi na mapambo kwa kimo cha (sm 140)”.

Kumbuka kuwa mradi huu unajengwa ili kupunguza msongamano ambao hutokea sehemu hiyo, na kuifanya iweze kupokea idadi kubwa zaidi ya mazuwaru, hususan katika siku za ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ambazo huwa na msongamano mkubwa, kiasi husababisha baadhi yao kushindwa kuingia ndani ya Ataba tukufu, ukizingatia kuwa hii ni moja ya sehemu mbuhimu ambayo hutumiwa na mazuwaru kutokana na nafasi ya mlango huu katika nafsi za watu wanaokuja kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: