Kuanza kwa kikao cha kwanza kwa lugha ya kiengereza katika kongamano la kielimu na kimataifa Al-Ameed awamu ya tano

Maoni katika picha
Jioni ya Alkhamisi mwezi (5 Safar 1442h) sawa na tarehe (22 Oktoba 2020m) mada ya kwanza ya kitafiti imeanza kuwasilishwa kwa lugha ya kiengereza, ambayo ni sehemu ya ratiba ya kongamano la kielimu na kimataifa Al-Ameed awamu ya tano, linalo simamiwa na kituo cha utafiti cha kimataifa, chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya kauli mbiu isemayo (Tunakutana katika ukumbu wa Al-Ameed kwa maendeleo) na kwa anuani ya (Selibasi ya kufundishia na tafiti.. kuithibitisha, kuihalili na kuiandaa), kupitia jukwaa na (Zoom).

Kikoa kimeongozwa na Profesa Haidari Ghazi Mussawi na kilikuwa na mada tano zifuatazo:

Mada ya kwanza imetolewa na Dokta Kristofa Tendiil kutoka chuo kikuu cha Winsord Kanada, inasema: (Nyenzo za fikra katika kutafiti agenda za kujadili sifa za selebasi).

Mada ya pili imetolewa na Dokta Zishani kutoka India, inasema: (Haja ya selebasi mpya katika ulimwengu wa kiislamu).

Mada ya tatu imetolewa na Dokta Maryam Safihi kutoka chuo kikuu cha Baabil, inasema: (Kupima selebasi na matokeo katika uhalisia wa ngazi ya elimu ya msingi.. darasa la tano katika shule za Iraq).

Mada ya nne imetolewa na Dokta Hussein Hawiliy kutoka chuo kikuu cha Dhiqaar, inasema: (Muingiliano wa lugha huwezesha kuingiliana kwa tamaduni na mambo mengine).

Mada ya tano na ya mwisho imetolewa na Dokta Mannaar Karim kutoka chuo kikuu cha kiislamu katika mji mtukufu wa Najafu, inasema: (Utafiti kuhusu selebasi ya lugha ya kiengereza katika shule za Iraq).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: