Kuhitimisha vikao vya uwasilishaji wa mada kwa lugha ya kiengereza katika kongamano la kielimu na kimataifa Al-Ameed awamu ya tano

Maoni katika picha
Jioni ya Jumamosi mwezi (6 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na tarehe (24 Oktoba 2020m), tumemaliza vikao vya uwasilishaji wa mada kwa lugha ya kiengereza katika kongamano la kielimu na kimataifa Al-Ameed awamu ya tano, linalo simamiwa na kituo cha Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, jumla ya vikao vitatu vyenye maza zinazo husu uboreshaji wa selebasi za masomo vimefanyika na kupata mwitikio mkubwa kutoka ndani na nje ya Iraq.

Vikao vimeongozwa na Profesa Haidari Ghazi Mussawi, jumla ya mada nne zimewasilishwa kama ifuatavyo:

Mada ya kwanza inasema (Sehemu muhimu katika kuboresha selebali) imewasilishwa na Dokta Hani Abadi kutoka Iraq.

Mada ya pili inasema (Mitihani ya lugha ya kiengereza ya darasa la tatu mutawasitwa) imewasilishwa na Ustadhi Warakaa Awadi Alwaailiy kutoka Iraq.

Mada ya tatu inasema (Kutengeneza selebasi kwa ajili ya jamii husika) iliyo wasilishwa na Jeska Ashi kutoka Marekani.

Kikao kikafungwa na mada ya nne isemayo (Nguvu iliyo jificha katika selebasi) iliyo wasilishwa na Dokta Shiri Wilyamson muandishi wa ulimwengu wa watoto.

Baada ya hapo Profesa Haidari Mussawi akatoa shukrani kwa watafiti walio wasilisha mada zao, kwa uwasilishaji mzuri, na wao wakawashukuru washiriki kwa ushirikiano mzuri pamoja na waandaaji wa kongamano hili, kutokana na mazingira ya sasa imelazimika kongamano kufanywa kwa njia ya mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: