Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Askariy (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi na imejaa huzuni na majonzi kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s), aliyekufa siku kama ya kesho Jumanne ya mwezi nane Rabiul-Awwal.

Bendera za huzuni zimepandishwa na vitambaa vilivyo andikwa ujumbe unao ashiria kuomboleza vimewekwa ndani ya haram tukufu, kama sehemu ya kuonyesha huzuni waliyo nayo waumuni katika nyoyo zao na kumpa pole Mtume (s.a.w.w) na Ahlulbait wake (a.s) kutokana na msiba huu mkubwa uliotokea mwaka wa 260h.

Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yake kwenye tukio kama hili, imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu.

Kumbuka kuwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kila sehemu ya dunia, wanaomboleza msiba huu na kumpa pole Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f) kwa kufiwa na baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s), alilala kitandani kwa siku kadhaa akiugulia huku akiwa ni mwenye kusubiri, aliuwawa akiwa na umri wa miaka ishirini na nane, alikufa mwezi nane Rabiul-Awwal mwaka wa (260h).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: