Kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi nane Rabiul-Awwal ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (s.a), naye ni Maasumu wa kumi na tatu na Imamu wa kumi na moja katika Maimamu wa Ahlulbait (a.s) baada ya Mtume (s.a.w.w), anaitwa Imamu Hassan bun Ali bun Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s).

Alizaliwa Rabiu-Thani mwaka wa 232h na akafa kishahidi mwaka wa 260h, akiwa na umri wa miaka 28, yeye ni miongoni mwa Maimamu walio kufa wakiwa na umri mdogo, Imamu Jawadi (a.s) alikufa akiwa na miaka 25, ameitwa Askariy kutokana na kuishi sehemu za askari katika mji wa Samaraa (kaskazini ya Iraq) aliishi hapo pamoja na baba yake Imamu Ali Alhaadi (a.s).

Riwaya zinaonyesha kuwa Imamu Hassan Askariy (a.s), alichukua jukumu la Uimamu baada ya kifo cha baba yake Imamu Ali Haadi (a.s) mwaka wa (253h), watawala wa Abbasiyya hawakumuacha huru Imamu Hassan Askariy (a.s), walimuweka chini ya ulinzi mkali wakati wote, walifuatilia harakati zake zote, Imamu alitumia njia ya siri kuwasiliana na watu wake.

Wakati wa Uimamu wake (a.s) alikutana na watawala wa Bani Abbasi wafuatao: Mu’tazu, Muhtada na Mu’tamadi, watawala hao watatu kila mmoja katika zama zake, alimtesa Imamu (a.s) na kumnyanyasa, alikuwa anatekwa mara kwa mara na watawala hao, mtawala wa mwisho alikuwa ni Mu’tamadi, alikuwa anapenda starehe na uovu hadi watu walimchukia kwa uovu wake.

Imamu (a.s) alinyanyaswa sana na Mu’tamadi, alimuwekea ulinzi mkali, askari wa Mu’tamadi waliwazuwia watu kukutana nae, yote hayo walifanya kutokana na husda kwa Imamu Askariy (a.s) na kuogopa asije akazaliwa Imamu Mahadi msubiriwa (a.s), ambae walijua kuwa atazaliwa na Imamu Hassan Askariy (a.s).

Mwisho Mu’Tamadi akaagiza Imamu (a.s) apewe sumu kali, iliyo sababisha augue kwa siku kadhaa na hatimae akafa akiwa na umri wa miaka ishirini na nane, alikufa mwaka wa (260h).

Alizikwa pamoja na baba yake Imamu Haadi (a.s) katika nyumba yake (Sarra man ra-aa) makaburi yao hutembelewa na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na hutabaruku kwao na kumuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: