Kuratibu majlisi ya kuomboleza katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wameratibu majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) ambaye kumbukumbu ya kifo chake inasadifu siku ya Jumanne mwezi nane Rabiul-Awwal, kwenye ukumbi wa Aljuud (uwanja wa mkabala na mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi -a.s-), chini ya utekelezaji wa masharti yote ya afya yaliyo tolewa na wizara ya afya na kusisitizwa na Marjaa Dini mkuu, majlisi hizo zitaendelea kwa muda wa siku tatu asubuhi na jioni.

Kiongozi wa idara Shekh Abdu-Swahibu Twaiy ameuambia mtandao wa Alkafeeel kuwa: “Ufanyaji wa majlisi hizi na zingine zinazo husu kukumbuka mazazi au kifo cha Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kunaingia chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) wa kuhuisha matukio, likiwemo tukio hili linalo umiza roho za wapenzi na wafuasi wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika siku kama hizi”.

Akaongeza kuwa: “Majlisi ya kuomboleza itaendelea kwa muda wa siku tatu, kuanzia mwezi sita Rabiul-Awwal, kutakuwa na mihadhara miwili kila siku, mmoja unatolewa asubuhi saa kumi na mbili na Shekh Mahadi Twarafiy na wa pili unatolewa jioni na Sayyid Ammaar Aali Yushaá mbele ya watumishi wa malalo takatifu na mazuwaru watukufu, kulingana na watu wanaoweza kuenea sehemu hiyo kwa kuzingatia ukaaji wa umbali kati ya mtu na mtu”.

Akabainisha kuwa: “Mihadhara hiyo imejikita katika historia ya Imamu Askariy (a.s), kwa kueleza mambo mbalimbali katika uhai wake (a.s) na mchango wake kwa umma wa kiislamu, pamoja na kuonyesha nafasi kubwa ya kuasisi zama za ghaiba ya Imamu wa zama (a.f)”.

Akahitimisha kwa kusema: “Majlisi hizi hufanywa kila mwaka katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Askariy (a.s) ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), lakini kutokana na mazingira ya sasa tunayo ishi mwaka huu ya janga la maambukizi ya virusi vya Korona, ambavyo tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuondolee balaa hili kwa baraka za tunaemkumbuka, majlisi imelazimika kufanywa katika eneo hili ambalo kitengo cha utumishi kimechukua jukumu la kufanya usafi na kupuliza dawa pamoja na maandalizi yote kwa ujumla”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: