Atabatu Abbasiyya tukufu inashuriki katika mkakati wa amani na kutoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Askariy (a.s) katika mji wa Samaraa

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa, kila mwaka hushiriki katika mkakati wa kulinda amani na kutoa huduma katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) katika mji mtukufu wa Samaraa, wafanyakazi wa kitengo cha utumishi na wale wa kitengo cha kulinda nidham, huenda kutoa huduma kwa mazuwaru.

Kitengo cha utumishi kimetuma idadi kubwa ya wahudumu wake kwenda kufanya kazi mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kupuliza dawa, kufanya usafi na kugawa maji, kimetuma idadi kubwa ya gari za kugawa maji (RO) katika mji mtukufu wa Samaraa, pamoja na gari za kufanya usafi na mifuko ya kuwekea taka.

Kuhusu kitengo cha kulinda nidham, watumishi wake wamekwenda kusaidia kuweka usalama na kusimamia mazingira ya ufanyaji wa ziara, kwa kusambaza watumishi wake wanao wasiliana moja kwa moja na Atabatu Askariyya pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama ndani na nje ya haram tukufu, wanafanya ukaguzi na kuratibu matembezi ya mazuwaru.

Kumbuka kuwa hii ni miongoni mwa ziara kubwa katika mji mtukufu wa Samaraa, idadi kubwa ya watu huja katika malalo ya Askariyyain (a.s) kufanya ziara na kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s), kwa ajili ya kusaidia kufanikisha ziara hiyo Atabatu Abbasiyya hushirikiana na Atabatu Askariyya kuwahudumia mazuwaru watukufu kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: