Kiwanda cha chakula cha kuku kimesema kuwa: Bidhaa zetu zinafika kila mkoa wa Iraq tena kwa ubora mkubwa

Maoni katika picha
Kiwanda cha chakula cha kuku Alwaahah kimepata mafanikio makubwa katika sekta ya ufugaji wa kuku, kwenye uzalishaji wa chakula cha kuku na usambazaji, kimefungua maduka katika mikoa mingi ya Iraq yanayo saidia kufikisha bidhaa zake kwa wafugaji wa kuku, sambamba na kuwa kiunganishi baina ya wafugaji na kiwanda.

Mkuu wa kiwanda Ustadh Hamidi Majidi amesema kuwa: “Kiwanda cha kutengeneza chakula kinatumia malighafi zenye ubora mkubwa, zinazo kiwezesha kutengeneza chakula cha kuku chenye ubora mkubwa”.

Akafafanua kuwa: “Kutokana na kazi nzuri inayofanywa na kiwanda cha kutengeneza chakula cha kuku Alwaahah, kimefanikiwa kutoa ushindani mkubwa kwa viwanda vya kigeni, bidhaa zetu zimejenga uaminifu mkubwa kwa wateja wetu, jambo ambalo limesababisha wafugaji wa kuku kutumia zaidi bidhaa zinazo zalishwawa na kiwanda chetu, ambazo ubora wake umethibitishwa na mamlaka ya wataalamu”.

Akasisitiza kuwa: “Tofauti ya bidhaa zetu na zingine ni ubora mkubwa unaopatikana kwenye chakula cha kuku kinacho tengenezwa na kiwanda chetu, jambo ambalo limepelekea kutumiwa zaidi na wafugaji wa mkoa wa Waasitu na kusini, ubora huo unatokana na uzowefu na umahiri wa wataalamu wetu, madaktari, wahandisi na wakulima”.

Akaongeza kuwa: “Kiwanda cha Alwaahah kina mitambo ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza chakula bora kabisa cha kuku, malighafi zinazo tumika zinakaguliwa ubora wake kila wakati, na bidhaa tunazo tengeneza zimekidhi viwango vya ubora wa kimataifa na ubora wake umethibitishwa na vipimo vyote”.

Kwa maelezo zaidi: tembelea kiwanda cha Alwaahah/ Karbala tukufu/ eneo la Ibrahimiyya.

Au piga simu: 07809182784 – 07809181581
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: