Hivi karibuni kituo cha turathi za kiislamu kimetoa kitabu cha (utukufu wa kiongozi wa waumini)

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za kiislamu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu cha (utukufu wa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib a.s), kutokana na kazi ya msomi mkubwa wa hadithi (Hafidhu bun Asaakir) Taqi-Dini Abu Qassim Ali bun Hibatu-Llahi bun Abdullahi Dimashqiy Shamiy (499 – 571h).

Kitabu kimehakikiwa na (Masudi Mahadi Zaadah), chini ya uangalizi wa (Ustadh Shekh Qais Bahajat Atwari) na kurejewa na kituo cha turathi za kiislamu, kitabu kina jumla ya kurasa (159).

Makamo rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu Shekh Ali Asadi amesema kuwa: “Utukufu wa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) unagonga masikio ya vizazi na vizazi, pamoja na kufichwa kwa muda mrefu, hakika ushia katika miji ya Sham –makazi ya ibun Asaakir Dimashqiy- una mizizi imara pamoja na kusalitiwa na bani Umayya, kupitia baadhi ya maswahaba na matabii wa karne ya kwanza, kama vile Abu Dhari Ghifari na Maliki Ashtari, walio tengwa na kupelekwa huko katika nyakati tofauti, wakawa wanahadithia watu utukufu wa kiongozi wa waumini na Ahlulbait (a.s), bila kusahau athari za mateka baada ya tukio la Karbala, kupitia mkakati wa Sajjaad (a.s) na Hauraa Zainabu (a.s), na watu kuangalia baadhi ya matukio, ushia ukakita mizizi katika mji wa Alepo na Sham kwa ujumla”.

Akafafanua kuwa: “Kutokana na umuhimu wa jambo hili, kituo cha turathi za kiislamu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, kimehakiki kitabu hiki chenye juzuu mbili zilizo jaa utukufu wa kiongozi wa waumini (a.s), kimehakikiwa na Ustadh Masudi Mahadi Zaadah na tumekipitia, kazi imekamilika”.

Kitabu hiki ni sehemu ya vitabu vya turathi vilivyo kusanywa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, kwa lengo la kuhuisha turathi za kiislamu, na kuchangia katika kuzipa vitabu maktaba za turathi pamoja na kuwasaidia watafiti kupata sehemu ya kurejea katika tafiti zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: