Kitengo cha malezi na elimu kinajadili mkakati wa masomo ya mwaka mpya wa masomo

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya maandalizi maalum ya kuanza mwaka mpya wa masomo, kimefanya vikao kadhaa vya kujadili mambo mbalimbali kwa ajili ya kuandaa mkakati mzuri wa masomo, utakao tekelezeka kwa urahisi, hususan katika mazingira haya ambayo taifa linapitia kwa sasa.

Dokta Ahmadi Kaabi rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya amesema: “Viongozi wa kitengo wamekutana na idara za shule za Al-Ameed, kujadili mkakati wa mwaka mpya wa masomo, na kuangalia namna ya kuondoa changamoto ambazo hukwamisha kazi, ukizingatia kuwa mwaka huu unatofautiana sana na miaka iliyopita, kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, wanafunzi wataenda shuleni kwa muda mfupi tofauti na ilivyo zoweleka, na kutegemea zaidi ufundishaji wa kutumia mitandao”.

Akafafanua kuwa: “Tumefanya vikao vingi kwa ajili ya kutafuta utatuzi wa changamoto unao endana na mazingira ya sasa, ukizingatia kuwa shule za Al-Ameed zilipata mafanikio makubwa katika miaka iliyopita, pamoja na mwaka huu wenye mazingira tofauti na miaka ya nyuma”.

Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya kazi kubwa ya kufundisha kwa njia ya mtandao, na kunufaika kwa kiwango kikubwa na teknolojia za kisasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: