Wakufunzi wa Alkafeel wanaendelea na kutoa mafunzo ya uokozi na huduma ya kwanza

Maoni katika picha
Wakufunzi wa Alkafeel wanaendelea kutoa mafunzo ya uokozi na huduma ya kwanza katika Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi saba kwa sababu ya janga la maambukizi ya virusi vya Korona. Wamefungua semina ya hamsini ambayo wameshiriki wapiganaji wa Hashdu-Shaábi, pamoja na kufuata kanuni zote za uokozi na huduma ya kwanza vitani (TCCC), sambamba na kutekeleza masharti ya idara ya afya.

Ustadh Murtadhwa Ghalibi mkuu wa wakufunzi wa Alkafeel amesema kuwa: “Semina hii ni ya hamsini kwa wapiganaji wa Hashdu-Shaábi na itadumu kwa muda wa siku saba, washiriki wapo (20) na watafundishwa kwa nadhariyya na vitendo, chini ya ratiba maalum ya kuokoa majeruhi vitani”.

Akaongeza kuwa: “Waokozi wanategemewa kimataifa na kuna kundi litasimamia utowaji wa maelekezo”.

Akamaliza kwa kusema: “Selebasi ya semina itahusisha masomo ya nadhariyya na vitendo katika uokozi wa majeruhi wa vitani, pamoja na mbinu za kuondoa majeruhi katika uwanja wa vita na mbinu zingine za uokozi anazohitaji mtoa huduma ya kwanza wakati wa kumtibu majeruhi kwenye uwanja wa vita”.

Kumbuka kuwa wakufunzi wa Alkafeel wamesha fundisha semina nyingi za mambo mbalimbali yanayo husiana na fani zao, makumi wa washiriki wamehitimu mafunzo hayo na kupewa vyeti vinavyo kubalika na vyama vya uokozi wa majeruhi vitani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: