Wanafunzi wa chuo cha Al-Ameed wanafanya msafara wa kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo katika mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia kitengo cha kuelekeza nafsi na mafunzo ya tarbiyya, wanafunzi wake wanashirikiana na taasisi ya Ain kutoa misaada kwa familia za watu wenye kipato kidogo katika mkoa wa Karbala, familia ambazo zimeathirika na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, hii ni sehemu ya misafara mingi waliyofanya siku za nyuma au waliyoshiriki katika utendaji wake.

Mkuu wa kamati ya utendaji Dokta Hasanaini Mussawi amesema kuwa: “Kutokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo, na maendeleo mazuri ya wanafunzi wa chuo sambamba na kufanyia kazi sera ya kusaidiana kijamii, chini ya ratiba ya wanafunzi ya kutatua changamoto za jamii au kuzitafutia ufumbuzi, tumefanya msafara huu ulio husisha familia zilizo kuwa na haja kubwa ya kusaidiwa, misaada hii itasaidia japo kwa kiwango kidogo kupunguza shida zao”.

Akasema: “Msafara huu ni sehemu ya kuonyesha kuwapamoja na familia za watu wenye kipato kidogo katika mazingira haya magumu, tunawapa moyo na kuwasaidia vyakula vya aina tofauti na baadhi ya vitu muhimu katika nyumba kutokana na michango ya wanafunzi, pamoja na kuwaonyesha kuwapenda na kuwajali katika mazingira haya magumu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: