Kuanza shindano la (Nabii Rahmah s.a.w.w) shindano la Quráni kwa njia ya mtandao upande wa wanawake

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu inaendesha shindano la (Nabii Rahmah s.a.w.w) kwa njia ya mtandao, kwa wasichana wenye umri wa miaka (10) hadi (17), linahusisha kuhifadhi moja ya sura zifuatazo (Muhammad –s.a.w.w-, Al-Muzammilu, Al-Mudathiru) pamoja na kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume mtukufu, Maahadi imetoa wito wa kushiriki kwenye shindano hilo.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa Maahadi tawi la wanawake bibi Manaar Jawadi Muhammad Aljaburi, akaongeza kuwa: “Shindano linafanywa kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (Meet), na unaweza kujisajili kupitia link ifuatayo: https://bit.ly/34vCpQq na link ya kushiriki shindano hilo ni: https://meet.google.com/myy-syae-fxd shindalo litafanyika siku ya Jumanne, tarehe (3 Novemba 2020m) sawa na mwezi (16 Rabiul-Awwal 1442h) saa tatu asubuhi”.

Kumbuka kuwa lengo la kufanya shindano hili ni kutambua watoto wenye uwezo wa kuhifadhi na kuwashajihisha waendelee kujifunza Quráni na kuhifadhi, ukizingatia kuwa sura zilizo chaguliwa zinabaadhi ya sifa za Mtume (s.a.w.w), aidha shindano hili ni sehemu kusherehekea mazazi yake, sura hizo zimetaja kazi kubwa aliyo fanya ya kuongoza umma na kulingania katika dini ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: