Katibu mkuu wa Atabatu Askariyya awapa zawadi watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Askariyya Mheshimiwa Shekh Abdusataar Murshidi, amewapa zawadi watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walio shiriki kuwahudumia mazuwaru wa malalo mbili za Askariyyaini (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s).

Kikao cha kukabidhi zawadi kimehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini pamoja na kiongozi wa idara ya utumishi na makamo rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu.

Zawadi hiyo ni sehemu ya kuthamini kazi kubwa waliyo fanya wakati wa ziara tukufu, Ataba zingine pia zimepewa zawadi hiyo, kama vile Atabatu Alawiyya, Kadhimiyya, Mazaru za kishia, Masjid Kufa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji.

Wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo kilicho fanywa ndani ya ukumbi wa utawala, Shekh Murshidi ameshukuru na kupongeza kazi nzuri iliyo fanywa na kuleta mafanikio makubwa, washiriki wametoa huduma za aina tofauti na wameshirikiana bega kwa bega na watumishi wa Atabatu Askariyya tukufu katika kuwatia nguvu ya kuwatumikia Ahlulbait (a.s), akamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awabariki watumishi wote.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesaidia kazi katika Atabatu Askariyya, imetoa huduma ya ulinzi, matibabu na huduma za kibinaadamu, jambo hilo linakuza ushirikiano na Ataba zingine pamoja na mazaru tukufu, na linasaidia kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa ardhi hii takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: