Uzinduzi wa dirisha la Mja Mwema Athibu Alyamani maarufu kwa jina la (Swafi-Swafa)

Maoni katika picha
Alasiri ya Ijumaa mwezi (12 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na (30 Oktoba 2020m) umefanyika uzinduzi wa dirisha la mja mwema Athibu Alyamani maarufu kwa jina la (Swafi-Swafa) katika mkoa wa Najafu Ashrafu.

Dirisha hilo limetengenezwa na mafundi na wahandisi wanaofanya kazi katika kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi matukufu na milango chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Katibu maalum wa mazaru ya Swafi-Swafa bwana Abdulhassan Shinuna, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tunaishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutengeneza dirisha hili, lililo tengenezwa kwa ikhlasi na umakini mkubwa chini ya mafundi wa kiiraq tunao jivunia”.

Akabainisha kuwa: “Dirisha hili ni mafanikio mengine yanayo ongezwa kwenye mafanikio ya Iraq, ambayo ni sehemu ya kazi adimu kufanywa”.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Ali Swaffaar amesema kuwa: “Hakika dirisha hili limetengenezwa na mafundi wanaofanya kazi katika kitengo cha utengenezaji wa madirisha na milango chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akasisitiza kuwa: “Hili sio dirisha la kwanza baada ya kutengenezwa durisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), bali walitengeneza dirisha la malalo ya Shekh Mufiid na Shekhe Tusi, pamoja na kutengeneza na kuweka dhahabu dirisha la maimamu wawili Kadhimaini (a.s) na dirisha la Qassim mtoto wa Imamu Mussa bun Jafari (a.s), na dirisha la Maqaam Imamu Mahadi (a.f) na kazi inaendelea ya kutengeneza dirisha lingine pia, kunadirisha linaendelea kutengenezwa la mkono wa kulia wa Abulfadhil Abbasi (a.s), hali kadhalika utengenezaji wa dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) bado unaendelea”.

Akaongeza kuwa: “Dirisha hili ni sehemu ya mafanikio mengine ya Iraq na Ataba tukufu, hususan Atabatu Abbasiyya inayo tekeleza mradi huu”.

Kumbuka kuwa lengo la kuanzishwa kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi na milango mitukufu ni kukidhi haja ya Atabatu Abbasiyya tukufu na Ataba zingine pamoja na mazaru takatifu za Iraq, kwa kutengeneza madirisha na milango maalumu kwa ajili ya Ataba na mazaru hizo, sambamba na kutunza alama za asili zilizo kwenye vitu hivyo ikiwa ni pamoja na dhahabu, watumishi wote wa kitengo hiki ni raia wa Iraq, wanafanya kazi kwa ukamilifu bila kusaidiwa na watu kutoka nje ya taifa, wanavifaa vyote vinavyo hitajika katika kazi hiyo, ikiwa ni pamoja na kitengo cha dhahabu ambacho kinatekeleza miradi yote inayo husisha dhahabu, wana vitendea kazi vya kisasa zaidi, kiwanda kina matawi mengi, kila tawi lina jukumu maalum, wanapo fanya kazi mpya kiwanda huandaa kila kitu kinacho tengenezwa kwa dhahabu na fedha katika haram tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: