Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inafanya nadwa kuhusu athari ya historia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa vijana

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume wa mwisho na muokozi wa binaadamu, Mtume Muhammad bun Abdullahi (s.a.w.w), maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa wito kwa wadau wote wa historia ya Mtume (s.a.w.w) washiriki kwenye nadwa itakayo fanyika kwa njia ya mtandao chini ya anuani isemayo: (Mwanga wa malezi kutoka katika historia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) – watoto na vijana kama mfano), mtoa mada atakuwa ni Dokta Amali Alhusseini.

Nadwa hiyo itaendeshwa kupitia mtandao wa (meet), mwezi kumi na saba Rabiul-Awwal 1442h, sawa na tarehe (4 Novemba 2020m) saa tatu jioni.

Mkuu wa Maahadi Ustadhat Mannaar Jaburi amesema kuwa, ratiba hii ni sehemu ya harakati za Maahadi katika kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w), inalenga kuangazia historia yake na kunufaika na mwenendo wake.

Nadwa itafanyika kipitia program ya (meet) kwa link ifuatayo:

https://meet.googel.com/bgh-xgzj-pqv
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: