Masomo ya vitendo kwa wanafunzi wa kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Al-Ameed kufidia yaliyo wapita katika mwaka wa masomo uliopita

Maoni katika picha
Kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Al-Ameed tangu siku ya (31/10/2020) kimeanza kufundisha kwa vitendo wasomo ya udaktari wa meno, kufidia pengo la mwaka jana lililosababishwa na kusimama masomo hayo kwa sababu ya janga la Korona, lililo athiri kila sekta ya maisha hususan sekta ya elimu.

Masomo hayo yamejikita katika tiba ya meno na kinywa, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata dozi kamili ya masomo, waliyo yakosa kipimdi cha ufundishaji kwa njia ya mtandao kutokana na janga la Korona.

Mkuu wa kitivo cha udaktari wa meno Dokta Basim Mutábu Zawin amesema kuwa: “Tumeanza kutoa masomo ya vitendo kwa wanafunzi wa kitivo cha udaktari wa meno, sambamba na kuheshimu maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa na kuheshimu umbali kati ya mtu na mtu”.

Akaongeza kuwa: “Wanafunzi tumewagawa makundi manne ya kuingia maabara, kwa kufuata ratiba iliyo wekwa na uongozi wa chuo, kwa ajili ya kupunguza msongamano baina yao pamoja na kuzingatia masharti ya kujikinga na virusi vya Korona”.

Akafafanua kuwa: “Chuo kikuu cha Al-Ameed kinavifaa vya kisasa vya kufundishia pamoja na juhudi kubwa ya walimu wanao hakikisha wanafunzi wanapata kile walichopoteza mwaka jana”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: