Chuo kikuu cha Alkafeel kimetangaza kufungua mlango wa shahada ya dokta na masta

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufungua mlango wa shahada ya dokta na masta, kama ifuatavyo:

  • 1- Famasiya (dokta / masta).
  • 2- Vifaa tiba (dokta / masta).
  • 3- Famasiya ya vitanda (dokta / masta).
  • 4- Kemiya ya viumbe hai (masta).
  • 5- Elimu ya uhai / falsaja (masta).
  • 6- Uhandisi wa kompyuta (masta).

Muombaji anatakiwa kukamilisha sifa zilizo wekwa na chuo, maombi yanaanza kupokelewa tarehe (1/11/2020) hadi (10/11/2020).

Kwa anayetaka kujiunga na masomo hayo afike katika ofisi za chuo zilizopo Najafu Ashrafu, mtaa wa Nidaa – nguzo ya 23 karibu na jengo la makazi Amiraat akiwa na vitu vifuatavyo:

  • 1- Taarifa zake binafsi.
  • 2- Shahada ya kuhitimu chuo.
  • 3- Vitambulisho vyake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: