Wito wa kushiriki katika shindano la (Twaha) la Quráni kwa njia ya mtandao kwa wanawake

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa wito wa kushiriki kwenye shindano la Quráni liitwalo (Twaha Mtume wa Mwenyezi Mungu –a-s) litakalo fanywa katika kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w) na linalenga wasichana wenye umri wa miaka (18) na zaidi.

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jawadi Muhammad Jaburi amesema kuwa: “Shindano hili ni sehemu ya harakati za Maahadi yetu, mara nyingi hufanywa sambamba na kumbukumbu za mazazi matukufu ikiwa ni pamoja na mazazi haya ya Mtume mtukufu”.

Akafafanua kuwa: “Lengo la shindano hili ni kuwatambua wenye uwezo wa kuhifadhi na kuwashajihisha waweze kusoma vizuri na kuhifadhi, ukizingatia kuwa sura zilizo chaguliwa zinabaadhi ya sifa za Mtume mtukufu (s.a.w.w), shindano hili ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume mtukufu, sura hizo pia zimetaja kazi kubwa aliyofanya Mtume ya kuongoza umma, na jihadi kubwa ya kulingania Dini ya kiislamu”.

Akabainisha kuwa: “Shindano litafanywa siku ya Jumamosi mwezi (20 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na tarehe (7 Novemba 2020m) saa tatu kamili, kupitia jukwaa la (Meet), unaweza kujisajili kupitia link ifuatayo: https://bit.ly/3kzm3f2

Na linki ya kushiriki shindano ni: https://meet.google.com/woy-advv-nnm”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: