Daru Rasuulul-Aádham (s.a.w.w) inaangazia riwaya zinazo zungumzia kuzaliwa kwa Mtume katika nadwa ya kielimu na imetoa wito wa kushiriki kwenye nadwa hiyo

Maoni katika picha
Daru Rasuulul-A’adham (s.a.w.w) katika kituo cha Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufanya nadwa kubwa kwa njia ya mtandao itakayo jadili mazazi ya Mtume mtukufu, chini ya anuani isemayo: (Kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w) katika riwaya za kihistoria na riwaya za Ahlulbait –a.s-), jioni ya Jumatano (17 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na (4 Novemba 2020m) kupitia jukwaa la (ZOOM), unaweza kujiunga kupitia link ifuatayo: https://us02web.zoom.us/j/3740873005

Daru imetoa wito wa kushiriki kwenye nadwa hiyo. Mhadhiri atakuwa ni Dokta Abduljabaar Naaji Yasiri.

Mkuu wa Daru kokta Aadil Nadhiru Biri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Katika miaka ya nyuma Daru ilikuwa inaendesha program katika vyuo vitatu tofauti kila mwaka, progam ilikuwa inapambwa na tafiti za aina tofauti pamoja na kaswida na maneno mazuri ya kukaribisha neema hii tukufu, lakini mazingira ya mwaka huu (janga la Korona) yamezuwia utaratibu huo, tumeamua kufanya nadwa ya kielimu kwa kujadili mambo ya kihistoria, nayo ni riwaya zilizopo katika vitabu vya historia pamoja na riwaya za watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ambao ndio chemchem halisi ya kila kitu katika uislamu, anuani ya nadwa inasema (Mazazi ya Mtume –s.a.w.w- kutoka katika riwaya za kihistoria na riwaya za Ahlulbait –a.s-)”.

Akaongeza kuwa: “Katika nadwa hii Daru inalenga kuhimiza wasomi wafanye tafiti za kielimu katika historia ya kiislamu”.

Kumbuka kuwa Daru Rasuulul-Aádam (s.a.w.w) inafanya kila iwezalo katika jitihada zake kukusanya historia ya Mtume (s.a.w.w), na kutoa fursa kwa wasomi waweze kuandika tafiti za kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: