Kuhuisha kuzaliwa kwa Maswadiq wawili: Muonekano wa mapambo umetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Muonekano wa mapambo ya furaha umetanda ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuadhimisha mazazi ya Maswadiq wawili, Mtume Mtukufu na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s), ambao tarehe ya kuzaliwa kwao inasadifu siku ya Jumanne (4 Novemba 2020m) sawa na mwezi (17 Rabiul-Awwal 1442h).

Kuta na korido za Ataba zimepambwa na kubandikwa mabango yenye maneno mazuri ya kumpongeza mbora wa Mitume Abu Qassim Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Swadiq (a.s), na zimewashwa taa za rangi zilizo pendezesha haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kuweka mauwa na miti ya mapambo sambamba na kuandika maneno ya kutoa pongezi katika milango ya haram hadi kwenye uwanja mtukufu wa katikati ya haram mbili na kuelekea katika kilele cha furaha ndani ya Atabatu Husseiniyya takatifu.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kusherehekea mazazi haya, inayo endana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, ratiba hiyo inavipengele vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: