Usiku wa kuzaliwa Mtume na tabia njema

Maoni katika picha
Alfajiri ya mwezi kumi na saba Rabiul-Awwal baada ya siku hamsini na tano toka kuangamizwa kwa watu wa tembo, alizaliwa Mtume wa umma na muombezi wake Mtume mtukufu Muhammad (s.a.w.w), jua halijawahi kuchomoza katika siku yenye baraka na utukufu zaidi ya siku hiyo, Mitume na Manabii (a.s) walikuwa wanasubiri siku hiyo pamoja na Malaika, nayo ndio siku ambayo ujumbe wa Mwenyezi Mungu uliandaliwa kwa ajili ya umma wake, ni siku bora na tukufu mmno katika historia, kwa nini isiwe bora wakati ni siku ya kuzaliwa mpenzi wa Mwenyezi Mungu na mbora wa viumbe wake.

Shekhe Swaduqu amepokea kutoka kwa Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema: (Ibilisi –laana iwe juu yake- alikua anakwenda katika mbingu saba, alipo zaliwa Nabii Issa (a.s) akazuwiwa kwenda katika mbingu tatu, akawa anaenda katika mbingu nne, alipo zaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) akazuwiwa kwenda katika mbingu zote saba, na mashetani wakaanza kupigwa kwa vijinga vya moto, makuraishi wakasema: hiki ndio kiyama tulichokua tunasikia watu wa kitabu wakiongea).

Amru bun Umayya aliyekuwa mtu maarufu katika zama za ujinga, akasema: Angalieni nyota ambazo huongoza watu katika safari na hutumiwa kutambua majira ya kiangazi na masika, kama zikirushwa mtambue ni maangamizi ya kila kitu, na kama zikiendelea kuwepo na zikarushwa nyota zingine, mjue kuna jambo limetokea. Siku aliyo zaliwa Mtume (s.a.w.w) masanamu yote yalidondoka chini. Katika usiku huo jengo la Kisra lilipasuka na vitu kumi na nne vya mfalme vikavunjika, na moto wa wafursi ukazimika, ulikua una miaka elfu moja bila kuzimika, kiongozi mkuu wa wamajusi katika usiku huo akaota ngamia mwembamba anamvuta farasi mkubwa na kuzungushwa katika mji wao, na taji ya mfalme Kisra ikavunjika, katika usiku huo nuru iliangaza hijazi yote hadi mashariki.

Hakikubaki kitanda cha mfalme duniani ispokua kiliharibika, na mfalme alipata ububu hakuweza kuongea siku hiyo, makuhani hawakujua kitu na uchawi ulibatilika, mawasiliano ya wachawi yalikatika, makuraishi walitukuzwa sana katika waarabu, Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema: (Walisema Aala-Llah kwa sababu walikua katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu), bi Amina anasema: Mtoto wangu alipo zaliwa alishika ardhi kwa mikono yake kisha akainua kichwa na kuangalia juu, halafu ikatoka nuru iliyo angaza kila kitu, nikasikia kutoka katika mwanga sauti isemayo: Hakika umemzaa mbora wa watu mwite Muhammad, akaja Abdulmutwalib kumuangalia, akamchukua na kumuweka miguuni kwake halafu akasema: kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu ambye amenipa huyu mtoto mwema, utukufu wake ni mkubwa kushinda watoto wote.. kisha akamlinda kwa utukufu wa nguzo za Alkaaba, ibilisi akapiga kelele –laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake- mashetani wote wakakusanyika kwake na wakamuuliza: kipi kimekufadhaisha ewe bwana wetu?!

Akasema: Ole wenu mbingu na ardhi vimebadilika tangu leo usiku, limetokea tukio kubwa hapa duniani, halijawahi tokea tukio kama hili tangu alipo ondoka Issa mwana wa Maryam, nendeni mkaangalie ni tukio gani hilo, wakatawanyika wakaenda kutafuta kila sehemu halafu wakarudi na kusema: hatujaona kitu, Ibilisi akasema: hivi kweli hakuna kitu. Kisha akapiga kelele, Jibrilu akamuambia, unataka nini ewe maluuni. Nauliza kitu gani kimetokea ewe Jibrilu, Jibrilu akamuambia: Amezaliwa Muhammad (s.a.w.w), akasema: Je naweza kumrubuni? Jibrilu akasema: Hauwezi. Akasema Umati wake je? Jibrilu akasema: Ndio. Akasema nimeridhika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: