Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza shindano liitwalo (Kwa wakweli wawili tunaongoka), katika kuhuisha na kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s), litafanyika kwa muda wa siku mbili na kuhusisha wanawake wenye umri tofauti.
Mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim amesema kuwa: “Hakika shindano hili ni sehemu ya mfululizo wa mashindano yanayo simamiwa na kituo, aidha ni miongoni mwa harakati za kitamaduni zinazo saidia kutambulisha na kunufaika na kumbukumbu hii takatifu, ya kuzaliwa kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadig (a.s)”.
Akaongeza kuwa: “Tumezowea kufanya maadhimisho haya kwa njia ya kawaida na kuhudhuriwa na washiriki mbalimbali, lakini kutokana na mazingira ya mwaka huu, ya kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona tumetosheka na kufanya shindano hili, linahusisha aina mbili za maswali, aina ya kwanza ni maswali yanayo husu Mtume (s.a.w.w) na aina ya pili yanahusu Imamu Jafari Swadiq (a.s), lengo la maswali yote ni kuwatambulisha watukufu hao wawili kupitia njia ya maswali na majibu, kwa njia ya historia, hadithi na zinginezo”.
Akafafanua kuwa: “Unaweza kushiriki shindano hili kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/QwHHcTv9zYjrQ47F9 baada ya kuchambua majibu sahihi kutakua na washindi watano, na tumeandaa zawadi za kugawa kwa washindi hao”.