Wahudumu wa kisayyid wanawapokea mazuwaru kwa maneno ya pongezi na mauwa kama ishara ya sherehe ya kuzaliwa Mtume (s.a.w.w)

Maoni katika picha
Wahudumu wa kisayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanawapokea mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa maneno ya pongezi na mauwa mazuri, kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa wakweli wawili, Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Jambo hilo ni sehemu ya harakati za idara hiyo katika kuhuisha matukio ya kidini ya furaha, na tarehe za kuzaliwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), wahudumu wa kisayyid wamekuwa wakifanya hivyo kila mwaka, husimama katika milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na ndani ya haram yake tukufu na kugawa mauwa huku wakiwapongeza kwa tukio hilo muhimu katika Dini, kwa nini wasifanye hivyo wakati wanasherehekea kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambaye tarehe ya kuzaliwa kwake inaendana na siku aliyozaliwa mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Jambo hilo limepokelewa vizuri na kupongezwa sana na mazuwaru, wametoa shukrani nyingi kwa wahudumu, wakasema pamoja na udogo wa jambo hilo lakini linaacha athari katika nyoyo zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: