Hafla ya wanawake ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume mtukufu na mjukuu wake Swadiq (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya sherehe kubwa ya kukumbuka kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s), ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika Ataba tukufu, na kuhudhuriwa na kundi la mazuwaru, na kufuata kanuni zote za kujikinga na maambukizi.

Ratiba ya sherehe hiyo ilikuwa na vipengele vingi kuhusu tukio hilo na utukufu wake, ilifunguliwa kwa Quráni kisha ukasomwa utukufu na sifa za mbora wa walimwengu Muhammad (s.a.w.w) pamoja na historia ya Imamu Jafari Swadiq (a.s), na ukasisitizwa umuhimu wa kushikamana na mwenendo wake, halafu zikaimbwa kaswida zilizo eleza tukio hili tukufu.

Bibi Taghrida Tamimi makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika hafla hii ni kutekeleza kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu, Mwenyezi Mungu amrehemu atakaehuisha mambo yetu), nayo ni sehemu ya harakati ambayo imezowea kufanywa na idara yetu katika kuhuisha matukio kama haya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: