Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamemaliza kazi ya kusafisha kubba na minara ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya mkakati uliowekwa na kitengo hicho kulingana na mazingira ya hali ya hewa, inayo weza kuathiri vifuniko vya dhahabu vilivyo funika kubba hiyo, na kuhakikisha vinadumu kwa muda mrefu bila kuchakaa, sambamba na kuonyesha uzuri wake unao endana na utukufu wa mwenye malalo hii takatifu.
Kazi ya kusafishwa inafanywa kwa kutumia vifaa maalum visivyo haribu vifuniko vya dhahabu vilivyopo kwenye kubba na minara, yote hayo yanafanywa kwa kuzingatia muda na umakini wa kazi, hatua ya kwanza ya usafishaji wa kubba hilo imehusisha upande wa mashariki mkabala na mlango wa Furaat (Alqami), katika muelekeo wa mnara wa saa, kuanzia juu hadi chini, kuanzia sehemu ulipo mlingoti wa bendera takatifu hadi chini ya kubba, baada ya hapo ikaanza kazi ya kusafisha minara.