Kuanza kutengeneza dirisha la Maqaam ya mkono wa kushoto wa Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wanaofanya kazi katika kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitakatifu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanza kutengeneza dirisha jipya la Maqaam ya mkono wa kushoto wa Abulfadhil Abbasi (a.s) litakalokuwa na ubora wa hali ya juu, kazi hiyo itaingizwa katika orodha ya mafanikio ya kazi tofauti walizo fanya ndani na nje ya Iraq, tena kazi hizo zinafanywa na raia wazalendo wa Iraq.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Nadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kupata maelekezo kutoka kwa uongozi wa juu wa Atabatu Abbasiyya, mafundi wetu wameanza kazi ya kutengeneza dirisha jipya la Maqaam ya mkono wa Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kukubaliana muundo wa dirisha hilo pamoja na nakshi na mapambo yatakayo wekwa”.

Akaongeza kuwa: “Dirisha litakua la pembe nane, nalo ni dirisha la kwanza kutengenezwa kwa muundo huo, lina urefu wa (mita 3) na kimo cha (mita 2.85) ikiwa ni pamoja na sehemu ya juu, limetengenezwa kwa:

  • - Silva ya ujazo wa (ml 2).
  • - Kuna mikato ya madirisha pamoja na mlango wa dirisha, kila kimoja kinaukubwa wa (sm 190) na upana wa (mt 1), upande wa kulia na kushoto kuna nguzo yenye urefu wa (sm 98), sehemu ya chini kuna kitako cha pambo chenye ukubwa wa (sm 18,5) kinaunganisha sehemu ya chini na nyingine yenye ureshu wa (sm 15) na sehemu ya juu inaungana na sehemu ya (taji la juu linalo fanana na taji la chini kimuundo) linaukubwa wa (sm 16.5), kuna ufito wa maandishi ya shairi wenye urefu wa (sm 60), idadi ya mapambo hayo imefika (16).
  • - Dirisha limezungukwa na nguzo pande zote, kila nguzo inaurefu wa (sm 154) na nguzo zipo (8) zimewekwa mapambo ya mimea na zinauimara mkubwa, zina silva ya ujazo wa (sm 28), na mwisho wa kila nguzo kuna mstari wa maandishi ya mashairi senye upana wa (sm 11).
  • - Sehemu ya juu inaukubwa wa (sm 75) na inamambo yafuatayo:

Kwanza: Kuna ufito wa maandishi ya Quráni wenye ukubwa wa (sm 20) umezunguka dirisha pande zote na umeandikwa aya isemayo (Hakika watu wema wapo katika neema…) hadi aya isemayo (…juu ya makochi wanaangalia) kwa wino wa dhahabu uliotiwa mina ya kijani, na kuna mstari wa mapambo umezunguka juu yake wenye ukubwa wa (ms 6).

Pili: ufito wa mapambo (uliotiwa dhahabu) umezunguka chuni ya madirisha unaukubwa wa (sm 28) kila uwa lina urembo wa duara, jumla kuna mapambo ya mauwa yapatayo (16), kila sehemu ya mapambo ya dhahabu inatenganishwa na ufito wa fedha kwenye nguzo zote za dirisha.

Tatu: ufito wa maandishi ya shairi wenye ukubwa wa (sm 20), katika mashairi yaliyo andikwa na Ali Swafaar, yameandikwa sehemu zinazo zunguka dirisha kwa wino wa dhahabu uliotiwa mina ya kijani.

  • - Chini ya dirisha kuna mapambo (8) yanayo tenganisha sehemu ya marumaru na dirisha ambayo yamewekwa juu ya kitako cha dirisha, na kufungamana na nguzo za dirisha kwa ndani.
  • - Ndani ya dirisha kuna mbao zilizo nakshiwa na kuwekwa mapambo ambayo hayatofautiani na yale yaliyowekwa nje ya dirisha.
  • - Dirisha lina mlango wa pande mbili, upande mmoja una urefu wa (sm 107) na upana wa (sm 45), imewekwa nakshi za mimea na kuna pambo la pembe tatu”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi ya kutengeneza dirisha hili bado inaendelea kama ilivyo pangwa, kazi yote inafanywa na mafundi ambao ni watumishi wa kitengo hicho, kuanzia usanifu, utengenezaji hadi ufungaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: