Ugeni wa walimu wa chuo kikuu cha Alkafeel unatembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Ugeni kutoka chuo kikuu cha Alkafeel ulio husisha rais wa chuo hicho na wakufunzi wake, umetembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kuangalia huduma zinazo tolewa na miradi hiyo kwa mazuwaru na jamii.

Rais wa chuo Dokta Nuris Dahani amesema kuwa: “Katika miradi hiyo tumeona utendaji mzuri wa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awawezeshe kuhudumia jamii yetu ya wairaq, ambayo inahitaji sana huduma hizo na kazi ya kila muiraq mwenye uwezo”.

Akaongeza kuwa: “Chuo kinalenga kunufaika kielimu kupitia ziara hii, kwa kuunda kamati za wataalam zitakazo fuatilia utendaji wa mambo ya kielimu kati ya miradi na chuo”.

Akasisitiza kuwa: “Miradi hii inatokana na uhakiki wa watendaji wa Atabatu Abbasiyya, wanao husika na kuhudumia jamii na kutatua changamoto”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu hupokea wageni kutoka vyuo vikuu kila baada ya muda na kubadilishana elimu na maarifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: