Kuanza kwa semina ya (Mubashiru) ya sauti na naghma inayo simamiwa na Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s), tumeandaa semina ya (Mubashiru) ya sauti na naghma inayo endeshwa na Maahadi ya Quráni tawi la wanawake, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongozi wa idara ya habari wa Maahadi Dokta Israa Akarawi amesema kuwa: “Hakika kutumia jina la (Mubashiru) katika semina hii kunatokana na kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambayo Maahadi imezowea kuyaadhimisha kwa kufanya shughuli mbalimbali zinazo husu Quráni”.

Akaongeza kuwa: “Maahadi imechagua wanafunzi (19) wenye umri wa miaka (10 hadi 17) baada ya kuwatahini, na kuwaingiza katika semina hii maalum ya sauti na naghma pamoja na maqamaat za Quráni, chini ya mkufunzi mahiri haafidhwah wa Quráni na msomaji bibi Hauraa Rawishdi, na kurekodi sauti nzuri za usomaji wa Quráni tukufu”.

Kumbuka kuwa semina hii ni moja ya harakati zinazo fanywa na Maahadi, miongoni mwa mfululizo wa harakati zinazo fanywa kwa ajili ya kushikamana na utamaduni wa Quráni tukufu katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: