Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimeanza hatua ya sita ya program ya (kitabu changu thamani yangu) ya wanawake kwa njia ya mtandao, ni program inayo himiza usomaji na kuongeza uwezo wa wanawake kielimu, na unalenga wanawake wa umri tofauti, awamu hii ni matokeo ya mafanikio yaliyo patikana katika awamu zilizo tangulia, uongozi wa kituo umepanga kuendeleza program hii.
Haya ndio yaliyosemwa na kiongozi wa kituo hicho bibi Asmahani Ibram, akaongeza kuwa: “Mtu anaye nyoosha mkono maktaba kwa ajili ya kuchukua kitabu na kusoma hiyo ndio akili, tusome vitabu vya hekima na mawaidha ili tupate nuru na kuondoa giza, ndio maana tunaendesha program ya (kitabu changu thamani yangu), program hii ni kinara kwa wanawake, huulizwa maswali yanayo chochea maarifa na kuongeza uwezo wa kielimu wa washiriki katika maisha yao ya kila siku”.
Akabainisha kuwa: “Muda wa kushiriki katika shindano hilo ni siku (15) za kusoma na kufanya mtihani, kutakuwa na zawadi za washindi watatu baada ya kupigia kura majibu sahihi”.
Washindi wataambiwa baada ya kuisha shindano na kuchambua ajibu sahihi.
Kumbuka kuwa program hii inakusudia kuamsha moyo wa kujisomea na kuongeza maarifa na uwezo wa kubadilika, chini ya uwelewa na maarifa salama.