Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kimeanza kutengeneza kizuwizi cha kimkakati kuanzia mji wa Ar-ur hadi Nakhibu

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) kimeanza kutengeneza kizuwizi cha udongo na handaki kuanzia Ar-ur hadi kitongoji cha Nakhibu katika hatua ya kwanza, zitafuata hatua zingine chini ya mkakati huo, ili kuimarasha ulinzi na kuhakikisha halitokea tukio la uvunjifu wa amani.

Kazi hiyo inafanywa chini ya maelekezo ya viongozi wakuu wa jeshi, na kwa kushirikiana na viongozi wa opresheni za pamoja na kikosi cha Karbala tukufu, na kushiriki kikosi cha opresheni ya Karbala na msaada wa moja kwa moja kutoka Atabatu Abbasiyya na wizara ya ulinzi.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: Utengenezaji wa kizuwizi ni kazi ya kimkakati inayo fanywa na kikosi, inalenga kuzuwia makungi ya kigaidi na kukata mawasiliano yao katika jangwa hilo la magharibi, uzio huo ni muhimu sana katika mkakati wa ulinzi hapa Iraq, utasaidia kulinda eneo kubwa la jangwa linalo karibia theluthi ya jangwa lote la hapa nchini.

Akaongeza kuwa: Urefu wa uzio wa kizuwizi hicho ni (km 120) na unakimo cha (mt 3) na upana wa (mt 4), handaki linaurefu wa (km 15), hadi sasa kazi imekamilika kwa asilimia %10 (m 1.30), watendaji wa mradi huo wanafanya kazi kwa bidii kubwa kwa ajili ya kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.

Nao viongozi wa kikosi wamesisitiza kuwa kazi hiyo itakamilika ndani ya muda uliopangwa, na wameiomba wizara ya maji ishiriki katika utendaji wa mradi huo.

Tambua kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinasimamia ulinzi wa amani katika eneo la (Karbala / Nakhibu) kwa zaidi ya miaka mitano, tangu wakati ule magaidi wa Daesh walipo teka maeneo ya mkoa wa Ambaar, chini ya maelekezo ya viongozi wa kikosi cha opresheni ya pamoja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: