Mawakibu zilizo chini ya idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu zimeadhimisha kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu bwana wa Mitume Muhammad (s.a.w.w), kwa kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo kutokana na michango ya wahisani watokanao na mawakibu hizo, kwa ajili ya kupunguza ugumu wa maisha katika mazingira magumu wanayo ishi.
Wameratibu misafara ya kwenda kugawa misaada katika mikoa kadhaa kupitia mawakibu zao chini ya ratiba maalum, kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara Qassim Maámuri amesema: “Mawakibu hazijaacha kutoa misaada kwa mafakiri na watu wenye kipato kidogo au kusaidia wapiganaji wa Hashdu-Shaábi na wanajeshi wa serikali, na katika sekta ya kuhudumia mazuwaru na kusaidia watumishi wa afya katika kupambana na janga la Korona”.
Akafafanua kuwa: “Kutokana na kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambaye ni kilele cha ukarimu na Mtume wa kudumu, maukibu zimegawa chakula (kibichi) pamoja na nguo kwa familia za mayatima, hususan wale wanao ishi katika nyumba maalum za kulea mayatima, sambamba na kuweka soko la bure kwa familia za mayatima katika mazaru ya Salmani Muhammadi (r.a), lililo sheheni vitu muhimu wanavyo hitaji kama vile chakula, mavazi na vinginevyo”.
Akaendelea kusema: “Kazi haikuishia hapo, bali kulikua na hafla pamoja na vikao vya usomaji wa Quráni tukufu kwa ajili ya kuhuisha mazazi haya matukufu”.