Kuratibu warsha ya kielimu yenye mada tofauti kwa vijana wa mkoa wa Muthanna

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni Al-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa harakati zake za kitamaduni, kimeandaa warsha ya kielimu kwa vijana wa mkoa wa Muthanna kutoka vitongoji tofauti.

Warsha imefanywa ndani ya ukumbi wa Qassim katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na rais wa kitengo tajwa Dokta Sarhani Jafaat, inaingia katika ratiba ya Multaqa inayodumu kwa muda wa siku tatu.

Makamo kiongozi mkuu wa kituo Ustadh Farasi Shimri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Washiriki wa warsha hii ni zaidi ya vijana 45 wenye umri na milengo tofauti ya kijamii, wamejadili mambo mbalimbali yaliyotatua baadhi ya changamoto za kitamaduni na kijamii pamoja na kujibu shubuhati (mambo tata), aidha kulikua na muhadhara kuhusu namna ya kutafakari”.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika warsha imejadili kuhusu mitandao ya mawasiliano ya kijamii, na athari yake katika kutengeneza fikra na kuzieneza, mitandao hiyo sio makini, ni mitandao ya kutumia majina tu”.

Naye Hussein Aamir Yahya amesema: “Tunashukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Multaqal-Qamaru kwa kufanya warsha hii iliyojibu maswali mengi ya vijana, jambo hili sio geni kwa Ataba tukufu, hakika imekua mstari wa mbele katika kufundisha maadili mema kwa vijana”.

Kumbuka kuwa Multaqal-Qamaru ni mradi unao lenga kufundisha vijana wa umri tofauti na kuelekeza namna ya kupambana na changamoto za kidini, kitamaduni, kijamii kwa kutumia njia za kielimu bila kutumia nguvu wala chuki, mambo ambayo huwa na matokeo mabaya na huleta madhara katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: