Kituo cha turathi za Hilla kimetoa jarida la kumi na nne la (turathi za Hilla)

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla kimetoa jarida la kumi na nne la (turathi za Hilla) –nalo ni toleo maalumu la Shekh ibun Idrisa Alhilliy-.

Tumeongea na mjumbe wa wahariri wa jarida hilo Dokta Iyadi Hamza Wishawi kuhusu jarida hilo, amesema kuwa: “Toleo hili limejaa tafiti za kisekula, kwani linatafiti za kina kuhusu vitabu vyote vilivyo andikwa na Shekh Hilliy na athari zake zilizo chapishwa, kuna tafiti kuhusu aya za mambo ya Aqida, pamoja na nafasi ya utambuzi katika uwanja wa Fiqhi, na sekta ya lugha na asili ya maneno, na maarifa mbalimbali pamoja na mafuhumu ya jihadi na mambo ya kihistoria na mengineyo”.

Akaongeza kuwa: “Kamati ya washauri na wahariri wa jarida la turathi za Hilla, zimefanya kazi kubwa ya kutoa machapisho maalum ya mambo muhimu katika turathi za wanachuoni wa Hilla, kwa kukusanya turathi zao mbalimbali walizo acha, kwa hiyo tumeona ni vizuri tuelekee katika tafiti za kisekula, kuanzia majina ya Allamah na historia yake sambamba na –kulifanya toleo hili kuwa la kumuelezea Shekh Ibun Idrisa Alhiliy kuanzia majina na historia yake”.

Tambua kuwa kituo cha turathi za Hilla ni moja ya vituo vilivyo anzishwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kwa ajili ya kulinda turathi za umma wa kiislamu, kama sehemu ya kuingiza vitabu vya turathi katika maktba, na kuwapatia watafiti sehemu za kurejea katika kuandaa tafiti zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: