Kwa upasuaji wa aina yake.. madaktari wa hospitali ya Alkafeel wamefanikiwa kumtibu mgonjwa aliyekuwa amevunjika mfupa wa uso

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel, limefanikiwa kumtibu kijana aliyekuwa amevunjika mara kadhaa mfupa wa uso.

Daktari bingwa wa upasuaji wa uso katika hospitali hiyo Dokta Ridhwani Twaiy amesema kuwa: “Hakika madaktari wetu wamefanikiwa kuunga mfupa uliokuwa umevunjika kwenye eneo la juu ya jicho pamoja na mfupa wa paji la uso na pua kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka ishirini”.

Akaongeza kuwa: “Mgonjwa huyo alijeruhiwa kwenye ajali ya gari na akavunjika mara kadhaa mifupa ya uso wake”.

Akafafanua kuwa: “Baada ya kufanyiwa upasuaji afya yake imeimarika na sasa anaendelea vizuri”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa chini ya madaktari mahili kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hupokea madaktari bingwa wa magonjwa tofauti kila baada ya muda fulani sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hatua mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: