Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake kupitia idara ya masomo ya Quráni, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufungua mlango wa usajili kwa mwaka mpya wa masomo (2020 – 2021), usajili utafanywa kwa njia ya mtandao kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa Maahadi hiyo bibi Mannaar Jawadi Aljaburi, akaongeza kuwa: “Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake, imezowea kufundisha kwa wanafunzi kuhudhuria darasani katika ofisi za Maahadi au katika mkoa wa Najafu, na kwenye matawi yake yaliyopo kwenye mikoa tofauti, lakini kutokana na mazingira ya sasa masomo yanatarajiwa kufundishwa kwa njia ya mtandao (elimu masafa) kupitia jukwaa maalum la mtandao, chini ya wakufunzi mahiri wa masomo ya Quráni”.
Akabainisha kuwa: “Utajisajili kwa kujaza fomu kwenye mtandao ufuatao https://bit.ly/3k4Htje na mwisho wa kujisajili ni (1 Desemba 2020m)”.
Akafafanua kuwa: “Itatumika selebasi ya Quráni inayo tambuliwa na kutumiwa na Maahadi za Quráni, inamasomo ya hukumu za tajwidi, kanuni za usomaji, tafsiri na kuhifadhi pamoja na mambo mengine, watu watakubaliwa kujiunga kutokana na viwango vyao vya elimu”.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tawi la wanawake, inalenga kusambaza elimu ya dini kwa wanawake, ikitanguliwa na elimu ya Quráni tukufu, na kuandaa kizazi cha wanawake wasomi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, wenye uwezo wa kulingania kwa kutumia kitabu cha Mwenyezi Mungu kitukufu na sunna za Mtume wake na Ahlulbait (a.s).