Chuo kikuu Alkafeel kimetangaza nafasi za masomo za mwaka (2020 / 2021m)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ofisi zake za Najafu Ashrafu, kimetangaza nafasi za masomo katika vitivo vyake vya (Udaktari wa meno, Ufamasiya, teknolojia za afya na udaktari, kitengo cha teknolojia ya vipimo vya kidaktari, uhandisi wa teknolojia/ kitengo cha uhandisi wa kompyuta, Sheria) kwa mwaka wa masomo (2020 /2021m).

Maombi ya kujiunga na masomo yatafanywa kwa kujaza fomu maalum iliyo tangazwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Uongozi wa chuo umebainisha kuwa tangazo hili limetolewa kwa kufuata kanuni ya kwanza 2s ya muongozo wa kukubaliwa kwa mwanafunzi katika vyuo vikuu vya serikali na binafsi kwa mwaka wa masomo (2020 – 2021m), mwanafunzi lazima awe na alama (0.5) na zaidi ili aweze kushindanishwa na wenzake.

Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi za chuo katika mkoa wa Nafafu/ barabara ya (Najafu – Karbala) mkabala na nguzo namba 23/ mtaa wa Nidaa karibu na majengo ya makazi Amiraat, au tembelea mtandao wetu https://alkafeel.edu.iq na unaweza kupiga simu zifuatazo: 07601839901 na 07803880900.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kimesajiliwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu chini ya sharia namba (J /H /S /187 ya 1/ 2/ 2005).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: