Kitengo cha Dini kinabainisha haki za waliokufa kwa walio hai kupitia kitabu cha (Anisul-Amwaat)

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimebainisha haki za waliokufa kwa walio hai, na wanacho weza kufanyiwa katika maisha yao ya akhera, kwa kutoa kitabu kiitwacho (Anisul-Amwaat) kilicho andikwa na Shekh Aamir Karbalai.

Amebainisha kuwa: “Ni wazi kuwa uhusino wa maiti na aliye hai hauishi, Dini ya kiislamu na hata Dini zingine zimetaja uhusiano huo, na zimesisitiza mafungamano ambayo huendelea hadi siku ya kiyama, nayo ni miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu na kuwa sababu ya kuokoa wafu katika siku ya kiyama, siku ambayo mtu haitamfaa mali wala watoto”.

Akaongeza kuwa: “Uhusiano huendelea kuwepo japokuwa mwanaadamu hutoweka katika ulimwengu wa muili, kwani huendelea kuwepo, napenda kuwaambia wasomaji watukufu kuwa mwanaadamu huondoka duniani kwa muili wake na huendelea kuwepo kwa roho yake na athari zake na hubakia milele”.

Akafafanua kuwa: “Napenda kufafanua katika kitabu hiki kuwa watu waliokufa wanahaki kwa watu walio hai, nitaeleza baadhi ya haki hizo kama kufanyia kazi usia ulioachwa na marehemu, na kuheshimu maiti kama alivyo kuwa anaheshimiwa akiwa hai, haifai kuivunjia heshima, kuitukana na kuishutumu, familia yake na watu wake wanao mtegemea wanatakiwa wasaidiwe, kaburi lake linatakiwa kutembelewa na kusomewa dua na Quráni, pamoja na mambo mengine yaliyo tajwa ndani ya Quráni na hadithi za Mtume pamoja na maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.

Tambua kuwa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kila baada ya muda fulani hutoa kitabu kinacho elezea mambo mbalimbali ya dini, utamaduni na mengineyo, ukitaka kuona kitabu hiki pamoja na vingine unaweza kutembelea maonyesho ya vitabu katika kitengo cha Dini kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: