Kuanza kutengeneza madawati kwa ajili ya hatua ya pili

Maoni katika picha
Mafundi wa maktaba ya kiraia ya mashahidi na wafanyakazi wa kujitolea katika mkoa wa Basra chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Liwaau/26 Hashdu-Shaábi, wameanza hatua ya pili ya kutengeneza madawati hapa mkoani kwa kushirikiana na ofisi ya malezi na usimamizi wa walimu, kazi hiyo inafanywa sambamba na kuanza mwaka mpya wa masomo, na baada ya kukamilisha hatua ya kwanza ambayo walitengeneza madawati (800), pamoja na kukarabati madirisha, milango na mfumo wa kunawa mikono katika jumla ya shule tisa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na msemaji wa kikosi, akaongeza kuwa: hatua hii ni sehemu ya kukamilisha hatua zilizo tangulia, na itahusisha shule kadhaa, tunaanza na shule ya Othumani Ubaidi chini ya idara ya malezi ya Zuberi hapa mkoani, ambapo tutatengeneza madawati (50) na tutaendelea kufanya hivyo katika shule zingine chini ya utaratibu maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: