Idara ya Tahfiidh katika Maahadi ya Quráni tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha semina ya Quráni yenye washiriki (75), chini ya utekelezaji wa maagizo ya idara ya afya ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Imewekwa mikakati maalum ya kuendelea semina hizi kulingana na mazingira ya afya ambayo taifa linapitia kwa sasa, wanafunzi wamewekwa makundi madogo madogo kwa ajili ya kuhakikisha wanakaa kwa umbali unao takiwa kati ya mtu na mtu.
Tambua kuwa tawi la Maahadi katika mji wa Najafu linaendelea kutoa semina za Quráni bila kusimama.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaabamu katika Atabatu Abbasiyya imezowea kufanya harakati mbalimbali za Quráni kila mwaka.