Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimefungua maonyesho ya kwanza ya turathi nzuri

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Alasiri ya leo Jumatatu (29 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na tarehe (16 Novemba 2020m) kimefungua maonyesho ya kwanza ya turathi nzuri, chini ya anuani isemayo (Rehema ya uongofu).

Maonyesho yanafanyika katika uwanja wa katikati ya haram mbili na yataendelea kwa muda wa siku saba, kuanzia siku ya (29 Rabiul-Awwal) hadi (5 Rabiu-Thani) sawa na tarehe (16 – 22/11/2020m), yanahusisha mabango yanayo onyesha utukufu wa Mtume (s.a.w.w).

Rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu Shekh Ammaar Hilali amesema kuwa: “Maonyesho haya yanahusu historia na utukufu wa Mtume wa mwisho Muhammad (s.a.w.w) kutokana na sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwake iliyo fanywa siku chache zilizopita”.

Akafafanua kuwa: “Maonyesho yanazaidi ya mabango (70) ya kuchapwa na kuchorwa, kutofautiana kwa mabango hayo kunalenga kuangazia sekta tofauti za maisha ya Mtume (s.a.w.w) pamoja na kuangazia fani hii muhimu katika uislamu”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa malengo mengine muhimu ya maonyesho haya ni kushajihisha watu wenye vipaji vya uchoraji kuendeleza vipaji vyao na kuwafanya vijana waijali fani hiyo”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya harakati mbalimbali za Quráni na kitamaduni katika kipindi cha mwaka mzima, chini ya ratiba maalum ambayo huandaliwa na kitengo hicho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: