Shule za Al-Ameed zinakamilisha maandalizi ya mwisho ya kupokea wanafunzi wapya

Maoni katika picha
Shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zinafanya maandalizi ya mwisho ya kupokea mwaka mpya wa masomo utakao anza ndani ya siku chache zijazo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, chini ya maelekezo ya wizara ya malezi na kamati ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Rais wa kitengo hicho Dokta Ahmadi Kaábi amesema kuwa: “Kutokana na mazingira ya sasa, shule za Al-Ameed zimechukua hatua kadhaa za kulinda usalama na afya za walimu na wanafunzi, sambamba na kutekeleza maagizo ya wizara ya afya, ili kufanyia kazi maagizo ya idara ya afya tumesha fanya vikao na idara za shule na kujadili maandalizi hayo”.

Akaongeza kuwa: “Shule bado zinaendelea kujiandaa kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo, kwa kukarabati madarasa na kuandaa vifaa vyote vya lazima pamoja na mazingira ya shule kwa ujumla, pamoja na kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi na kutekeleza maelekezo ya wizara ya afya pamoja na shirika la afya la kimataifa katika kupambana na janga la Korona”.

Akamaliza kwa kusema: “Mkutano huo ulitanguliwa na mikutano mingi tuliyofanya na viongozi wa shule, kwa ajili ya kupamga mkakati maalum wa mwaka huu ambao unatofautiana na miaka mingine, kwa sababu idadi ya wanafunzi watakao hudhuria darasani itapunguzwa na watafundishwa pamoja na njia ya mtandao, kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: